Kuendelea
kung’ang’ania na kutaka matokeo unayataka yatokee kwenye maisha yako, naweza
kusema hili ni moja ya jambo la muhimu sana katika ujasiriamali. Iko wazi
utakutana na changamoto kwenye njia ya mafanikio, lakini huwezi kuchoka ni lazima
ung’ang’anie mpaka lile lengo lako liweze kutimia.
Unapokutana
na changamoto na ukaamua kuwa mbishi kwa kupambana nazo, hapo utakuwa upo
kwenye njia sahihi ya mafanikio yako. Wajasiramali walio wengi ni watu wa
kung’ang’ania na kwa sababu hiyo huwasaidia sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Ukishindwa kuwa king’ang’anizi sahau mafanikio ya ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment